Tuesday, March 4, 2014

Wema Sepetu aharibu hafla ya Pastor Muyamba


Superstar wa Bongo movie Wema Isaac Sepetu  aka Beutiful Onyinye  hivi karibuni alimuharibia siku Emanuel Myamba maarufu kama Pastor Muyamba, kwa kushindwa kufika kwenye hafla iliyokuwa imeandaliwa na chuo chake cha sanaa ‘TFTC’ akiwa kama mgeni rasmi.
 
Wema Sepetu.
Mtoa habari wetu ndani ya taasisi hiyo aliliambia gazeti hili kuwa, Wema aliombwa na kukubali kuhudhuria shughuli hiyo, lakini alipopigiwa simu dakika za mwisho aliwaambia kwamba atashindwa kufika kwa kuwa amefiwa na shangazi yake udhuru ambao baadaye ulibainika kuwa haukuwa wa kweli